Huduma Zetu
Huduma za Tafsiri na Ukalimani
Baraza hutoa huduma ya tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya umma na binafsi, asasi za kitaifa na kimataifa na watu binafsi. Kuhusu tafsiri, Baraza lina wataalamu wa lugha mbalimbali zikiwamo Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kiarabu, Kireno, Kichina, Kirusi, Kijapani, Kihispaniola, n.k.
Huduma ya tafsiri hutozwa kiasi kidogo cha gharama kwa ajili ya kazi zinazoambatana na ukamilishaji wake.
Kuhusu huduma ya ukalimani, Baraza lina kanzidata ya wataalamu waliobobea katika kazi hiyo na linaratibu upatikanaji wao kwa ajili ya mikutano ya kitaifa na kimataifa.
