Sehemu ya Istilahi na Kamusi

Majukumu ya Sehemu hii ni: -

  1. Kuandaa msamiati na istilahi zinazotakiwa kusanifishwa, kuratibu usanifishaji wake na kuzisambaza;
  2. Kuandika kamusi za jumla na mahususi kwa ajili ya matumizi ya taaluma  mbalimbali;
  3. Kufanya utafiti  kuhusiana na kamusi na istilahi mbalimbali;
  4. Kuandika makala na maandiko mengine kuhusiana na kamusi na istilahi; Kutoa mafunzo ya muda mfupi ya uandaaji wa kamusi na istilahi kwa wanaohitaji; na
  5. Kukusanya maneno kutoka kwenye maandiko ya Kiswahili na kuyaingiza kwenye Kongoo ya Kiswahili ya Taifa.