Sehemu ya Utumishi na Utawala

Majukumu ya Sehemu hii ni kama ifuatavyo: -

  1. Kutafsiri sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya huduma na kushauri utekelezaji wake;
  2. Kuandaa na kutoa mafunzo kwa  watumishi;
  3. Kuandaa na kusimamia mishahara ya watumishi;
  4. Kusimamia mfumo wa usimamizi wa taarifa za kiutumishi na mishahara za wafanyakazi wa BAKITA 
  5. Kusimamia mipango ya mafao na fidia kwa watumishi;
  6. Kuratibu uundaji na utendaji kazi wa Baraza la Wafanyakazi;
  7. Kusimamia masuala ya nidhamu mahali pa kazi;
  8. Kusimamia shughuli zote za kiutawala ofisini;
  9. Kutoa huduma na msaada wa kisheria;
  10. Kutunza nyaraka zote za kisheria za Baraza; na
  11. Kusimamia tafiti za kisheria na kuushauri vyema utawala wa Baraza.