Sehemu ya Lugha, Fasihi na Uhariri
Majukumu ya Sehemu hii ni: -
- Kupitia na kutoa ithibati ya matumizi sahihi ya Kiswahili katika maandiko mbalimbali;
- Kutoa mafunzo ya Kiswahili kwa wageni;
- Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa makundi yenye mahitaji mbalimbali kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili;
- Kutoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu mbinu za uandishi na uhariri kwa wanaohitaji.
- Kuandika makala na maandiko mengine kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili;
- Kufanya tafiti na kutoa machapisho kuhusu fasihi ya Kiswahili;
- Kuhariri vitabu, miswada na maandiko mengine ya Kiswahili;
- Kuandaa mashindano ya uandishi wa lugha ya Kiswahili katika ngazi mbalimbali za elimu;
- Kuendesha na kuratibu mafunzo kwa wanafunzi wanaofanya kazimradi zinazohusiana na lugha ya Kiswahili; na
- Kuratibu na kuendesha maonesho ya utamaduni.
