Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
Majukumu ya Kitengo hiki ni kama ifuatavyo: -
- Kuandaa na kutekeleza mpango- mkakati wa TEHAMA;
- Kutoa ushauri kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia zenye gharamu naafu;
- Kuandaa na kusimamia makavazi ya kielektroni kwa ajili ya kutunza nyaraka na kumbukumbu muhimu za Baraza;
- Kutoa huduma endelevu za msaada kwa watumiaji;
- Kuunda na kusimamia mifumo ya uhifadhi na urejeshaji wa data za Baraza;
- Kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao ili kuhakikisha uzingatiaji wa sera, sheria na viwango vya TEHAMA serikalini,; na
- Kuandaa, kukusanya na kuhifadhi takwimu za Baraza.
