Sehemu ya Tafsiri na Ukalimani
Majukumu ya Sehemu hii ni:-
- Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Kuratibu na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya kujenga na kuimarisha uwezo wa wafasiri na wakalimani kitaifa na kimataifa;
- Kuandika makala na maandiko mengine yanayohusiana na tafsiri na ukalimani;
- Kuandaa na kuhuisha kanzidata ya wafasiri na wakalimani ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa lengo la kuwakutanisha na fursa pindi zinapotokea;
- Kuthibiti ubora wa kazi za tafsiri na ukalimani;
- Kupitia na kuthibitisha tafsiri zilizofanywa na taasisi zingine na mawakala wa BAKITA; na
- Kufanya tafiti zinazohusiana na tafsiri na ukalimani.
