Hatua ya Kati

Kozi ya Kati ya Kiswahili ni Muendelezo wa Misingi ya Lugha na Utamaduni wa Kiswahili Iliyojengwa kwa Ngazi ya Anza.

Kozi hii ni mwendelezo wa Kiswahili hatua ya awali, ambayo inatarajiwa kupanua kwa kiasi kikubwa msingi wa ujuzi wa Kiswahili alioupata awali na kumtambulisha kwa dhana na muhimu za kisarufi ili uweze kuwasiliana kwa ufanisi na kwa urahisi katika hali halisi na Maisha ya kila siku katika kijamii kwa kuzingatia utamaduni. Katika hatua hii, mjifunzaji atajihusisha na aina mbalimbali za matini halisi halisi za sauti na maandishi ya Kiswahili zinayokusudiwa kumwonyesha mitindo tofauti ya kuzungumza Kiswahili na kuongeza ufahamu wake wa kusikiliza na uwezo wa kushiriki katika mazungumzo na mijadala kuhusu mada mbalimbali. Pamoja na shughuli za darasani, utashiriki katika ziara za kimasomo na kiutamaduni, shughuli mbalimbali za kijamii zinazokupa uwezo wa kuzamia kindakindaki na kuipata na utamaduni wake. Hatua hii inalenga kutoa changamoto na kuimarisha ujuzi wa kuzungumza katika mazingira yasiyotabirika na yasiyopangiliwa ya lugha ya Kiswahili.

 

MBINU

Mbinu kuu ya ufundishaji katika Mwongozo huu ni mbinu shirikishi inayohusisha:

  1. Mkabala wa kimawasiliano
  • Maigizo
  • Ziara
  • Kazi za vikundi
  • Majadiliano
  • Nyimbo
  • Michezo ya lugha
  • Vitu halisi
  • Video/televisheni/sauti

 

  1. Uzamishaji
  • Familia mwenyeji
  • Rafiki wa lugha
  • Mazoezi kwa vitendo
  • Kumwalika mgeni
  • Kazimradi
  1. Ujifunzaji wa Hiari
    • Utafiti mdogo
    • Mapitio ya machapisho mbalimbali
    • Kazi za ubunifu

MJIFUNZAJI ATAJIFUNZA NINI?

Kuzungumzia njia za usafiri, Kuzungumza kuhusu miundombinu, Kuzungumza kuhusu huduma za jamii, Kungumza kuhusuhuduma za kifedha, Kuzungumza, kuhusu makazi (nyumba), Kuzungumza kuhusu Masuala ya uhifadhi wa mazingira, Kuzungumza kuhusu ujasiriamali, Kuzungumza kuhusu vikundi vya maendeleo ya jamii, Kuzungumza kuhusu mifumo ya elimu, Kuzungumzia Stadi zamaisha kwa vijana,Kuzungumza kuhusu mapishi ya Kitanzania.

WALENGWA WA KOZI HII NI WATU GANI?

Ni watu wenye ujuzi wa lugha ya Kiswahili na waliohitimu hatua ya awali, ambao wanaweza kuwa:

  • Wafanyakazi wa maendeleo,
  • wamisionari,
  • Madaktari,
  • Wafanyabishara,
  • Wawekezaji
  • wataalam kutoka nje ya nchi,
  • watafiti,
  • watalii,
  • wanafunzi na yeyote anayehitaji kujifunza lugha ya Kiswahili katika hatua ya kati.