Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini

Majukumu ya Sehemu hii ni:-

  1. Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Muda wa Kati, Mipango Kazi na Bajeti ya Mwaka kulingana na bajeti ya serikali;
  2. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango ya Baraza;
  3. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa miradi, programu mbalimbali, na mipango kazi;
  4. Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa programu za uwekezaji za Baraza;
  5. Kufanya tathmini ya shughuli mbalimbali za Baraza; na
  6. Kuandaa na kutekeleza mikakati ya uhamasishaji wa matumizi ya rasilimali