Huduma Zetu

Usanifishaji na Usambazaji wa Istilahi za Kiswahili

Usanifishaji na Usambazaji wa Istilahi za Kiswahili

Baraza husanifisha istilahi mbalimbali za lugha ya Kiswahili na kuzisambaza kwa watumiaji. Aidha, Baraza hutoa ushauri na  ufafanuzi kuhusiana na tafsiri sanifu za nyanja mbalimbali kwa watumiaji wa Kiswahili. 

Utaratibu wa usanifishaji, huhusisha watalaamu wa lugha ya Kiswahili na wataalamu wa nyanja mbalimbali zinazohusika. Wataalamu hao hupitia orodha ya istilahi mbalimbali za lugha za kigeni zilizokusanywa na BAKITA pamoja na zile zinazotoka kwa wadau wengine wa Kiswahili na kusanifisha visawe vyake vya lugha ya Kiswahili.

Baraza lina vitabu vya istilahi zilizosanifishwa za nyanja zifuatazo: Utawala na Menejimenti, Biolojia, Biashara na Uchumi, UKIMWI na Magonjwa husianifu, Agronomia na Ufugaji, Saikolojia, Saikatria, Michezo, Uhandisi Kilimo, Magonjwa ya Mimea/Wanyama na Wadudu Waharibifu, n.k.

Vitabu hivi vya istilahi husambazwa kwa watumiaji kwa njia mbalimbali kama vile, maonesho ya kitaifa na kimataifa, makongamano na mikutano na kutangazwa katika vyombo vya habari kama vile redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii.