Huduma Zetu
Ushauri kwa Wanafunzi na Watafiti
Baraza hutoa ushauri kwa wanafunzi wa Kiswahili wa ngazi zote wanaoandika kazimradi za kielimu na tasnifu za vyuo vikuu kuhusu makuzi na maendeleo ya Kiswahili. Aidha, Baraza hujibu hoja za watafiti na wachunguzi wa fani mbalimbali za Kiswahili.
