Huduma Zetu
Kutoa ithibati ya lugha
Kwa mujibu wa Sheria ya kuanzishwa kwa Baraza ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 1983 na 2016, mswada/kitabu chochote cha kiada au ziada kilichoandikwa kwa Kiswahili ili kutumika katika mfumo wa elimu nchini hakina budi kupata ithibati ya lugha kutoka Baraza. Kwa hiyo, mwandishi/mchapishaji wa mswada/kitabu chochote kinachokusudiwa kutumika katika mfumo rasmi wa elimu, anawajibika kukileta katika Baraza ambapo matumizi ya lugha hupitiwa. Baada ya Baraza kuhakikisha kuwa marekebisho yaliyopendekezwa yamefanywa, litatoa Cheti cha Ithibati ya Lugha ambacho huwasilishwa pamoja na mswada/kitabu Wizara yenye dhamana ya Elimu kwa ajili ya kuhakiki maudhui ya kitabu. Huduma hii hutolewa kwa gharama nafuu.
