Category Title
UTAMADUNI WA MTANZANIA WANG’ARA PARIS KUELEKEA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI
Maonesho ya Utamaduni wa Mtanzania yaliyofanyika jijini Paris, Ufaransa, yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani tarehe 7 Julai 2026.
Mgeni rasmi katika maonesho hayo alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Christian Makonda, akishirikiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Saidi Othman Yakubu, pamoja na viongozi wengine waliojitokeza kushuhudia urithi, mila, desturi na ubunifu unaoitambulisha Tanzania kimataifa.
Kupitia maonesho hayo, washiriki walipata fursa ya kujionea utajiri wa utamaduni wa Mtanzania kupitia mavazi ya asili, kazi za mikono, sanaa na vipengele mbalimbali vya urithi wa Kiswahili, huku shughuli nyingine za maonesho zikitarajiwa kuendelea kesho katika mwendelezo wa maadhimisho haya muhimu.
