Category Title
LUGHA YA KISWAHILI KUFUNDISHWA NCHINI URUSI
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kupitia Katibu Mtendaji wake, Bi. Consolata Mushi, pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi, Bw. Maxim Reshetnikov, wamesaini makubaliano ya ushirikiano kuhusu lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha zitakazofundishwa nchini Urusi.
Tukio hilo limefanyika lleo tarehe 16 Mei, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha wakati wa Kikao cha Tatu cha Tume ya Pamoja ya Kimataifa ya Ushirikiano wa Biashara na Uchumi kati ya Tanzania na Urusi, kilichowakutanisha viongozi wa serikali, wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka mataifa hayo mawili.
Aidha, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, alishuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo, huku Serikali ya Tanzania ikiendelea kuweka mkazo katika kukuza, kueneza na kuitangaza lugha ya Kiswahili kimataifa kama sehemu ya Utamaduni, Utambulisho na Diplomasia ya taifa.
