Category Title
MAANDALIZI YA KONGAMANO LA KISWAHILI LA KIMATAIFA YAENDELEA KUSHIKA KASI
Manaibu makatibu wakuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Bw. Methusela Ntonda na Bw. Makame Haji Machano (Zanzibar) ,wakiongoza kikao cha maandalizi kilichofanyika jana, tarehe 27 Aprili 2026 katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Posta jijini Dar es Salaam ambapo Kamati ya maandalizi imekutana kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha malengo ya kongamano hilo yanafikiwa
Kongamano linatarajiwa kufanyika jijini Paris, Ufaransa kuanzia tarehe 4 hadi 7 Julai 2026, sanjari na maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani (7 Julai 2026).
Lengo kuu ni kuimarisha hadhi ya Kiswahili kimataifa, kukuza matumizi yake katika elimu, biashara na teknolojia pamoja na kujenga mtandao imara wa wadau wa Kiswahili kutoka mataifa mbalimbali ili kuchochea ubunifu, tafiti na diplomasia ya lugha.
