Category Title
MISS WORLD APAMBWA KWA KHANGA, AENDA SOKONI
23 Nov, 2026
Mrembo wa Dunia (Miss World 2026), Joheirry Molla, amevalishwa khanga, vazi la asili linalotambulisha utamaduni wa Pwani, wakati akiendelea na ziara yake hapa nchini.
Miss Molla akiwa pamoja na warembo wenzake ametembelea kikundi cha Mamas of Zanzibar, kinachojihusisha na upishi wa vyakula vya asili pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Katika ziara hiyo, Miss World na wenzake pia wametembelea Soko la Chuini, Zanzibar, ambako wamenunua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya vyakula vya asili, ikiwa ni sehemu ya kujifunza na kufurahia utamaduni wa Tanzania.
