BAKITA LAWANOA WALIMU WA KISWAHILI KWA WAGENI MKOANI ARUSHA

13 Dec, 2025
BAKITA LAWANOA WALIMU WA KISWAHILI KWA WAGENI MKOANI ARUSHA

Washiriki wa Mafunzo ya Kuimarisha Stadi ya Kufundisha Kiswahili kwa Wageni, yaliyoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na kufanyika jijini Arusha kuanzia Desemba 1 hadi 5, wapokea vyeti vya utambuzi baada ya kukamilisha mafunzo hayo.

Aidha, wakufunzi 11 wa Kiswahili kwa Wageni kutoka jijini Arusha wametambuliwa rasmi na BAKITA kuwa Wakufunzi wa Kiswahili kwa Wageni kuanzia Desemba 2025.