BAKITA LAPOKEA MKAKATI WA TAIFA WA KUKABILIANA NA MMOMONYOKO WA MAADILI, LAWEKA MSUKUMO MPYA KWA MATUMIZI SAHIHI YA KISWAHILI

29 Apr, 2026
BAKITA LAPOKEA MKAKATI WA TAIFA WA KUKABILIANA NA MMOMONYOKO WA MAADILI, LAWEKA MSUKUMO MPYA KWA MATUMIZI SAHIHI YA KISWAHILI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Consolata Mushi  amekabidhiwa Mkakati wa Taifa  wa Kukabiliana na Mmomonyoko wa Maadili na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Christian Makonda leo tarehe 29/04/2026 Mtumba Jijini Dodoma, katika hafla fupi ya uzinduzi wa Mkakati huo.

 

Miongoni mwa dhamana kubwa za Mkakati huo ni kuhakikisha maadili ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mazungumzo na maandishi yanadumishwa.

 

Uzinduzi wa Mkakati huo umefanywa na Mheshimiwa Paul Christian Makonda Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dorothi Gwajima.