BAKITA LASHIRIKI MKUTANO WA EAC KUJADILI MAENDELEO YA KISWAHILI AFRIKA MASHARIKI

29 Oct, 2026
BAKITA LASHIRIKI MKUTANO WA EAC KUJADILI MAENDELEO YA KISWAHILI AFRIKA MASHARIKI

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), kupitia Katibu Mtendaji wake, Bi. Consolata P. Mushi, limeshiriki katika Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Mkutano huo unafanyika nchini Uganda kuanzia tarehe 27 hadi 31 Oktoba 2026.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa kuhusu maendeleo na matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani, Sera ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, pamoja na programu ya kubadilishana wataalamu (Mobility Programme) inayolenga kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu na ujuzi miongoni mwa wataalamu wa nchi wanachama.

Aidha, nchi ambazo bado hazijaanzisha mabaraza ya Kiswahili zilipewa fursa ya kueleza hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa maelekezo ya kuanzisha taasisi hizo. Kenya, Uganda na Rwanda zimeonesha maendeleo katika mchakato huo, ambapo nyaraka za kuanzishwa kwa mabaraza ya Kiswahili zimewasilishwa katika mabaraza ya mawaziri ya nchi husika kwa ajili ya kuidhinishwa.