BAKITA YATATHMINI UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU, YAWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA KISWAHILI

07 Oct, 2026
BAKITA YATATHMINI UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU, YAWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA KISWAHILI

Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Bw. Martin Mhando, akiongoza Kikao cha 15  cha Bodi ya Baraza pamoja na Katibu mtendaji  wa Baraza, Bi. Consolata Mushi. Kikao hicho kimefanyika leo, tarehe 07 Oktoba 2026, katika Ukumbi wa Baraza uliopo Kijitonyama, Dar es Salaam. Kikao hicho kinalenga kujadili na kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Baraza, maendeleo yaliyofikiwa pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha matumizi na maendeleo ya Kiswahili nchini.

 

Kikao hicho ni muhimu katika kuimarisha utendaji na mwelekeo wa kimkakati wa BAKITA, hususan katika kutekeleza jukumu lake la kukuza, kuendeleza na kusimamia matumizi sahihi ya Kiswahili. Aidha, maamuzi na mikakati inayowekwa na Bodi yana mchango katika utekelezaji wa sera na vipaumbele vya Serikali katika kukuza Kiswahili kama nyenzo ya Mawasiliano, Elimu, Utamaduni na Utambulisho Wa Taifa, sambamba na kuongeza matumizi na hadhi ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.