Category Title
BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA) LAHITIMISHA MAFUNZO YA KUIMARISHA STADI ZA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA WAGENI.
01 Aug, 2026
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limehitimisha mafunzo ya kuimarisha stadi za kufundisha Kiswahili kwa wageni yaliyofanyika kuanzia tarehe 20 Julai 2026 katika Ofisi zake zilizopo Kijitonyama, Dar es Salaam, yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kutumia mbinu bora za ufundishaji wa lugha ya Kiswahili.
Akifunga rasmi mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo na Matumizi ya Kiswahili Bw. Kulwa Abel Kindija, amewasihi washiriki kutumia maarifa na stadi walizozipata ili kuboresha ufundishaji wa Kiswahili na kuchangia katika ukuzaji, uenezaji na uendelezaji wa lugha hiyo katika maeneo yao ya kazi ili kuunga mkono juhudi za serikali za kukibidhaisha Kiswahili ndani na nje ya nchi.
