Category Title
MAFUNZO YA TAFSIRI
12 Aug, 2026
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) linawatangazia wadau mbalimbali kushiriki Mafunzo ya Tafsiri.
Lengo la Mafunzo haya.
- kuwajengea washiriki uwezo na stadi za kitaaluma katika kutafsiri matini mbalimbali.
Walengwa
- Wadau mbalimbali wenye lugha zaidi ya moja kutoka taasisi za Serikali, binafsi na watu wote wanaopenda kufanya kazi za tafsiri.
Muda na Mahali
📅 Tarehe: 07-18 Septemba 2026.
📍 Mahali: Ofisi za BAKITA-Kijitonyama
⏰ Muda: 08:00 Mchana– 11:00 Jioni
📞 Mawasiliano:
Simu: +255 657 734 266
Karibuni sana kushiriki mafunzo haya muhimu.
