Category Title

  • Hakuna Taarifa kwa sasa
  • Hakuna Taarifa kwa sasa

MAFUNZO YA KUIMARISHA STADI ZA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA WAGENI KANDA YA ZIWA – JIJINI MWANZA

10 Aug, 2026

Baraza la Kiswahili la Taifa linawatangazia Wataalam wa Lugha ya Kiswahili na Walimu ya lugha ya Kiswahili waliopo Jijini Mwanza na maeneo ya jirani mafunzo ya kuimarisha stadi za kufundisha Kiswahili kwa wageni ana kwa ana na  mtandaoni.

Mafunzo haya yanalenga:

  • Kuimarisha uwezo wa walimu wa Kiswahili kwa Wageni katika kutumia mbinu bora za ufundishaji zinazozingatia mahitaji na viwango mbalimbali vya wajifunzaji wa Kiswahili kwa wageni au kama lugha ya kigeni.
  • Kuwajengea washiriki uelewa wa matumizi sahihi ya teknolojia ikiwemo Akiliunde (AI) katika kuandaa na kutengeneza matini na zana kufundishia Kiswahili kama lugha na si kama somo.
  • Kuboresha uwezo wa walimu kuwawezesha wajifunzaji kuwasiliana katika mazingira halisi kwa kutumia stadi zote nne za lugha ambazo ni kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika kwa kutumia mbinu shirikishi na mkabala wa kimawasiliano.
  • Kuwatambua na kuwapa vyeti maalumu vya utambuzi wahitimu wa mafunzo hayo.

Walengwa:

  • Walimu wa Kiswahili wenye elimu ya kuanzia stashahada na kuendelea.
  • Wataalamu wa Lugha wanaofundisha Kiswahili kwa wageni lakini hawana cheti cha utambuzi kutoka BAKITA

Muda na Mahali

📅 Tarehe: 07- 11 Septemba 2026

📍 Mahali: Jijini Mwanza, katika Shule ya Sekondari Mwanza.

📝 Usajili: Kabla ya tarehe 01 Septemba 2026

Kujisajili bofya kiungo hiki:  https://forms.edodoso.gov.go.tz/x/5UIwH7Fs

📞 Mawasiliano:
Simu: +255 755 906 376 au +255 752 430 560
Barua pepe: edward.nnko@bakita.go.tz  au omary.machibya@bakita.go.tz

Karibuni sana kushiriki mafunzo haya muhimu.