Category Title
MAFUNZO YA MATUMIZI YA KISWAHILI FASAHA NA SANIFU KWA MAOFISA TEHAMA
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) linatangaza mafunzo maalum ya matumizi ya Kiswahili kwa Maofisa TEHAMA. Lengo la mafunzo haya ni kuongeza ujuzi wa matumizi ya Kiswahili fasaha na sanifu, pamoja na kuzingatia utamaduni wa lugha ya Kiswahili katika mawasiliano ya kikazi na kiutawala, hususan katika nyanja za teknolojia ya habari na mawasiliano.
Mafunzo haya yanalenga kuwajengea washiriki uwezo wa kutumia Kiswahili kwa usahihi katika uandishi, tafsiri, uhariri na mawasiliano yanayohusiana na masuala ya TEHAMA, ili kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mazingira ya kidijitali na kitaaluma.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa awamu mbili: awamu ya kwanza tarehe 04 hadi 09 Mei 2026, na awamu ya pili tarehe 11 hadi 16 Mei 2026, katika ukumbi wa Hoteli ya Morena, mkoani Morogoro.
Ada ya ushiriki ni ShT. 628,000/= BAKITA inawahimiza wahusika kujisajili mapema ili kupata nafasi.
Kwa maelezo zaidi na usajili, wasiliana nasi kupitia: 📞 +255 713 705 704
