Category Title

  • Hakuna Taarifa kwa sasa
  • Hakuna Taarifa kwa sasa

MAFUNZO YA MATUMIZI YA KISWAHILI SANIFU NA FASAHA KWA WAANDISHI WAENDESHA OFISI (WWO)

10 Aug, 2026

Moja ya majukumu ya msingi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni kusimamia matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili nchini Tanzania. Katika kutekeleza jukumu hilo, BAKITA linawatangazia Waandishi Waendesha Ofisi (WWO) kushiriki Mafunzo ya Matumizi ya Kiswahili Sanifu na Fasaha kwa Waandishi Waendesha Ofisi (WWO) yatakayofanyika Septemba 2026 jijini Tanga. Mafunzo haya yanalenga kuongeza na kuimarisha ujuzi katika matumizi ya Kiswahili Fasaha na Sanifu katika miktadha rasmi ikiwemo mahali pa kazi.Hii ni pamoja na kujua matumizi sahihi ya lugha kwa kuzingatia utamaduni wa Mswahili. Mafunzo haya yametoa kipaumbele kwa WWO kwa sababu wao ni moja ya makundi ya wafanyakazi ambao kazi zao zinahusisha sana uandaaji wa nyaraka mbalimbali za ofisi kama vile barua, kumbukumbu za vikao, taarifa, madokezo, n.k.

Malengo Mahususi ya Mafunzo

  • Kuboresha stadi za uandishi wa barua, kumbukumbu za vikao, taarifa mbalimbali, ripoti na nyaraka nyingine za kiofisi kwa kuzingatia kanuni za lugha ya Kiswahili sanifu na fasaha.
  • Kuwajengea Waandishi Waendesha Ofisi uelewa wa matumizi sahihi ya msamiati, sarufi, tahajia na matumizi sahihi ya viakifishi.
  • Kuwajengea uwezo wa kutambua  na kurekebisha makosa anuai ya Kiswahili sanifu na fasaha katika nyaraka mbalimbali.
  • Kuwajengea uwezo WWO wa kufanya uhariri mzuri wa nyaraka wanazoziandaa.
  • Kuimarisha uelewa wa matumizi ya herufi kubwa na ndogo.
  • Kuwaongezea ufahamu wa matumizi ya TEHAMA katika lugha ya Kiswahili.
  • Kuwapatia ujuzi wa msingi wa kutafsiri matini katika lugha mbili: Kiswahili na Kiingereza.
  • Kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili yenye weledi, usahihi na inayozingatia maadili, heshima na utamaduni wa Kiswahili katika mazingira ya kazi.

Uwezeshaji wa Mafunzo

Mafunzo haya yanaratibiwa na BAKITA ambapo walimu wenye weledi wa juu wanahusika katika kuwezesha mafunzo hayo kwa muda wiki moja. Washiriki wanafundishwa pamoja na kupewa mazoezi mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha mada wanazosoma. Baada ya mafunzo, washiriki waliohudhiria siku zote za mafunzo hupatiwa cheti cha ushiriki.

Muda na Mahali

Mafunzo haya yatafanyika jijini Tanga kwa awamu mbili:

📅 Tarehe: 07-12 Septemba 2026 (Awamu ya 1)

                       21-26 Septemba 2026 (Awamu ya 2)
Usajili &  Ada ya Mafunzo

Washiriki ambao ni WWO wanatakiwa kujisajili kupitia  https://tsms.gov.go.tz/login   kabla ya tarehe 05/09/2026. Ada kwa kila mshiriki ni ShT 600,000 endapo mshiriki hatahitaji kupewa Kamusi Kuu ya Kiswahili, na ShT 628,000 endapo mshiriki atahitaji kupewa kamusi tajwa. Ada hiyo itagharimia: uwezeshaji wa mafunzo, chamcha, chai ya asubuhi na jioni, ukumbi na vifaa vya mafunzo.

Mawasiliano

Kwa maelezo zaidi kuhusu mafunzo haya, wasiliana na Mratibu  wa Mafunzo, Dkt. Rizati Mmary kwa simu namba +255 713 705 704 na/au anwani ya baruapepe rizati.mmary@bakita.go.tz

Karibuni sana mushiriki katika mafunzo haya muhimu.