Category Title
MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAKALIMANI
10 Aug, 2026
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) linawatangazia wadau kutoka taasisi mbalimbali kushiriki Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Wakalimani. Mafunzo haya yanalenga kuwajengea washiriki maarifa na stadi za ukalimani wa kitaaluma kwa kuzingatia kanuni, maadili na mbinu za ukalimani, pamoja na matumizi sahihi ya Kiswahili sanifu na fasaha katika mawasiliano rasmi na mazingira mbalimbali ya kazi.
Mafunzo haya yanalenga:
Kuwajengea washiriki uelewa wa misingi, kanuni na maadili ya taaluma ya ukalimani.
- Kuimarisha stadi za ukalimani wa papo kwa papo na ukalimani mfululizo katika mazingira mbalimbali ya kitaaluma.
- Kuwajengea uwezo wa kuwasilisha ujumbe kwa usahihi, ufasaha na ukamilifu bila kupoteza maana ya lugha ya awali.
- Kukuza umahiri wa matumizi ya Kiswahili sanifu na fasaha katika shughuli za ukalimani.
- Kuwawezesha washiriki kutumia mbinu bora za usikilizaji, uchambuzi na uwasilishaji wa ujumbe wakati wa ukalimani.
- Kuwajengea washiriki uwezo wa kutumia istilahi sahihi za Kiswahili katika nyanja mbalimbali za kitaaluma wakati wa ukalimani.
- Kuwawezesha washiriki kutekeleza majukumu ya ukalimani kwa kuzingatia weledi, maadili ya taaluma na mahitaji ya mazingira ya kazi.
Walengwa
- Wakalimani na watafsiri wanaotaka kuimarisha umahiri wao wa kitaaluma.
- Watumishi wa umma na binafsi wanaotekeleza majukumu yanayohusisha ukalimani katika mikutano, semina, warsha na makongamano.
Muda na Mahali
📅 Tarehe: 05-16 Oktoba 2026.
📍 Mahali: Ofisi za BAKITA-Kijitonyama
⏰ Muda: 08:00 – 11:00 Jioni
📞 Mawasiliano:
Simu: +255 657 734 266
Karibuni sana kushiriki mafunzo haya muhimu.
