Tanzania emblem

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)

Tanzania emblem
Dondoo
Baraza la Kiswahili la Taifa kuendesha mafunzo ya Kuimarisha Stadi za Kufundisha Kiswahili kwa Wageni tarehe 20 hadi 24 Machi 2023.

Kuhusu BAKITA

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Shirika la Umma ambalo kwa kawaida huwa chini ya Wizara yenye dhamana ya Utamaduni. Baraza liliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 1983 na 2016. Sheria hii inalipa Baraza mamlaka ya kusimamia na kuratibu shughuli za wadau wote wanaokuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baraza liliundwa kutokana na mapendekezo makuu ya Kamati iliyoundwa kwenye kikao cha wataalamu wa lugha kilichoitishwa na Waziri wa Elimu Disemba 1961. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuinua Kiswahili kama lugha ya Taifa. Baraza lilianza kazi na watumishi wanne katika ofisi za Wizara ya Elimu. Miongoni mwa kazi ya kwanza ya Baraza ilipendekezwa iwe kufasiri msamiati na misemo ya Sheria. Baadaye mwaka 1972, Baraza lilipata ofisi zake katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa, mtaa wa Samora na Azikiwe jijini Dar es Salaam, na mwaka 2012 Baraza lilihamia Kitalu Na.45 B, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Huduma Zitolewazo na BAKITA

Huduma ya Ushauri kwa wanafunzi na watafiti

Soma Zaidi>>

Huduma ya Kutoa ithibati ya lugha

Soma Zaidi>>

Huduma za Tafsiri na Ukalimani

Soma Zaidi>>

Usambazaji wa Istilahi za Kiswahili

Soma Zaidi>>

Habari Mpya

  • 8th Feb 2023

MAFUNZO YA KISWAHILI KWA WAGENI

Soma zaidi
  • 8th Feb 2023

MATUKIOBARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA) KUWA NA KANZIDATA YA WATAALAMU WA KISWAHILI

Soma zaidi
  • 8th Feb 2023

MAFUNZO YA KUTAMBUA VIPAJI VYA UKALIMANI

Soma zaidi

Matangazo

Machapisho

15th Mar 2023 | publications
MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

Vitabu vya BAKITA

Maneno ya Mtandaoni

Neno: Udhalala

Maana: Ukosefu wa adabu na uadilifu katika mwenendo

Mfano:Udhalala haukubaliki katika jamii.

Neno: Diradira

Maana: Kwepa kusema ukweli kwa kuzungusha maneno

Mfano:Alidiradira alipokamatwa na polisi.

Neno: Oweza

Maana: Furahisha mtu baada ya kupata dhiki

Mfano:Aliowezwa baada ya nyumba yake kuungua