Tanzania emblem

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)

Tanzania emblem

Majukumu Mbalimbali ya BAKITA

Majukumu:

  1. Kukuza maendeleo ya matumizi ya lugha ya Kiswahili mahali pote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2. Kushirikiana na vyombo vingine katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo vinahusika na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili na kuratibu kazi zao
  3. Kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika shughuli za Serikali na kwa shughuli za umma
  4. Kuhimiza matumizi fasaha ya lugha ya Kiswahili na kuzuia Upotoshaji wake.
  5. Kushirikiana na mamlaka yanayohusika katika kuanzisha tafsiri sanifu ya istilahi za Kiswahili
  6. Kuchapisha gazeti au jarida la Kiswahili litakalohusika na lugha ya Kiswahili na fasihi yake
  7. Kutoa huduma kwa Serikali, mamlaka za umma na kwa waandishi binafsi waandikao kwa Kiswahili kuhusu Kiswahili.

  8. Kwa kushirikiana na vikundi vyovyote vya kimataifa, taasisi, au kundi la watu, na watu binafsi kufuatilia, kushauri na kuratibu shughuli zinazolenga kukuza Kiswahili.
  9. Kwa kushirikiana na kikundi, Taasisi na vyombo mbalimbali vya kitaifa kuratibu utafiti wa Kiswahili unaofanyika katika Jamhuri ya Muungano.
  10. Kwa ombi maalumu kutoka kwa waandishi au mfasiri yeyote, kuwa na jukumu la kuchunguza vitabu vya au maandishi yaliyoandikwa na kufasiriwa katika Kiswahili na kuhakikisha kwamba lugha iliyotumika ni sanifu na inakubaliwa na Baraza.
  11. Kushirikiana na wachapishaji, kusaidia waandishi waandike Kiswahili sanifu.
  12. Kuanzisha mashindano ya maandishi ya Kiswahili.
  13. Kwa kushirikiana na Wizara inayoshughulikia elimu, kuthibitisha vitabu vya kiada vilivyoandikwa kwa Kiswahili kabla ya kuchapishwa, kwa ajili ya Asasi za Elimu.