Sehemu za BAKITA
Majukumu ya sehemu hii ni:
- Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Kuratibu na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya kujenga na kuimarisha uwezo wa wafasiri na wakalimani wa ndani
- Kuandika makala na maandiko mengine kuhusiana na tafsiri na ukalimani
- Kuandaa kanzidata ya wafasiri na wakalimani ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Kudhibiti ubora wa kazi za tafsiri na ukalimani
- Kupitia na kuthibitisha tafsiri zilizofanywa na taasisi mbalimbali au mawakala wa BAKITA
- Kufanya tafiti za masuala ya tafsiri na ukalimani
Majukumu ya sehemu hii ni:
- Kuandaa msamiati na istilahi zinazotakiwa kusanifiwa, kuratibu usanifishaji wake na kuzisambaza
- Kuandika kamusi za jumla na mahususi kwa ajili ya matumizi ya taaluma mbalimbali
- Kufanya utafiti kuhusiana na kamusi na istilahi mbalimbali
- Kuandika makala na maandiko mengine kuhusiana na kamusi na istilahi; Kutoa mafunzo ya muda mfupi ya uandaaji wa kamusi na istilahi kwa wanaohitaji
- Kukusanya maneno kutoka kwenye maandiko ya Kiswahili na kuyaingiza kwenye Kongoo ya Kiswahili ya Taifa.
Majukumu ya sehemu hii ni
- Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Muda wa Kati, Mipango Kazi na Bajeti ya Mwaka kulingana na bajeti ya Serikali
- Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango ya Baraza
- Kuandaa ripoti za utekelezaji wa miradi, programu na ,mipango kazi
- Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa programu za uwekezaji za Baraza
- Kufanya tafiti za shughuli mbalimbali za Baraza
- Kuandaa na kutekeleza mikakati ya uhamasishaji wa matumizi ya rasilimali
Majukumu ya sehemu hii ni:
- Kupitia na kutoa ithibati ya matumizi sahihi ya Kiswahili katika maandiko mbalimbali
- Kutoa mafunzo ya Kiswahili kwa wageni
- Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watu wenye mahitaji maalumu kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili
- Kutoa mafunzo ya muda mfupi ya mbinu za uhariri kwa wanaohitaji
- Kuandika makala na maandiko mengine kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili
- Kufanya tafiti na kutoa machapisho kuhusu fasihi ya Kiswahili
- Kuhariri vitabu, miswada na maandiko mengine ya Kiswahili
- Kuandaa mashindano ya uandishi wa lugha ya Kiswahili katika ngazi mbalimbali za elimu
- Kuendesha na kuratibu mafunzo kwa wanafunzi wanaofanya kazimradi zinazohusiana na lugha ya Kiswahili
- Kuratibu na kuendeshaa maonesho ya utamaduni.
Majukumu ya Sehemu ya Uhasibu ni:
- Kukusanya na kusimamia mapato
- Kufanya upatanisho wa Kibenki
- Kuandaa Hesabu za Mwaka na Taarifa zingine za Kifedha
- Kushughulikia miamala ya fedha taslimu na hundi
- Kuweka kumbukumbu/kufanya upatanisho wa masurufu yote yanayotolewa
- Kujibu hoja za ukaguzi
- Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya Baraza kwa mwezi, robo, nusu na mwaka
- Kusimamia maandalizi ya kumbukumbu zote za hesabu na kuhakikisha kuwa zimewasilishwa mahali husika
- Kuandaa na kupitia kanuni za kifedha