Tanzania emblem

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)

Tanzania emblem

Maadili ya Msingi

Ili BAKITA liweze kukaa katika mazingira wezeshi kwa ajili ya kufikia malengo yake ya kukuza na kusimamia maendeleo ya Kiswahili ndani na nje ya nchi, yafuatayo yatakuwa maadili yake ya msingi:


  1. Kukuza ushiriki wa jamii: Kukuza ushiriki wa jamii kuhusu matumizi ya Kiswahili fasaha katika matumizi rasmi ya jamii
  2. Utendaji wa pamoja: Kufanya kazi kwa pamoja kama timu ili kufikia malengo ya Baraza na jamii kwa ujumla
  3. Kufanya kazi kwa bidii: Kuongeza juhudi katika kutoa huduma na kuzingatia ubora wa huduma zinazotolewa
  4. Uadilifu: Kuwa waadilifu na mfano wa kuigwa katika utendaji kazi
  5. Uwajibikaji: Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuzingatia ukuzaji na uimarishaji wa lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi
  6. Matumizi mazuri ya rasilimali: Kutumia kwa uangalifu rasilimali za Baraza kwa manufaa na maendeleo ya lugha ya Kiswahili
  7. Uwazi: Kuzingatia uwazi wakati wa utekelezaji wa majukumu na kuwa tayari kupokea maoni ya jamii
  8. Kukubali mabadiliko: Kuwa tayari wakati wote ili kuendana na mabadiliko