Vitengo Mbalimbali vya BAKITA
Majukumu ya Kitengo hiki ni kama ifuatavyo:
- Kuandaa na kutekeleza mpango- mkakati wa TEHAMA
- Kutoa ushauri kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia zenye gharamu naafu
- Kuandaa na kusimamia makavazi ya kielektroni kwa ajili ya kutunza nyaraka na kumbukumbu muhimu za Baraza
- Kutoa huduma endelevu za msaada kwa watumiaji
- Kuunda na kusimamia mifumo ya uhifadhi na urejeshaji wa data za Baraza
- Kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao ili kuhakikisha uzingatiaji wa sera, sheria na viwango vya TEHAMA serikalini
- Kuandaa, kukusanya na kuhifadhi takwimu za Baraza
Majukumu ya kitengo hiki ni kama ifuatavyo;
Kushauri kuhusu masuala ya kuanzisha kazi/biashara mpya, kukuza mitandao na ushirikiano kwa wabia wa kitaifa na kimataifa na kuvutia wateja katika huduma zinazotolewa na Baraza.
- Kuanzisha na kutekeleza mikakati ya masoko;
- Kutangaza na kuuzabidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na Baraza
- Kuhifadhi kumbukumbu za matukio yote ya Baraza
- Kupitia na kuhuisha taarifa katika tovuti na majukwaa ya mitandao yote ya kijamii
- Kupokea maswali, maombi na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali
- Kufanya utafiti wa masoko ya bidhaa na huduma zinazotolewa na Baraza
Majukumu ya kitengo hiki ni kama ifuatavyo
- Kuandaa mpango wa ukaguzi wa ndani wa Baraza
- Kuunda na kusimamia utekelezaji wa sera za ukaguzi wa ndani
- Kupendekeza maboresho ya utendaji kazi wa ndani ya Baraza
- Kufanya ukaguzi wa ndani katika maeneo yote ya shughuli za Baraza
- Kushirikiana na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali wakati wa ukaguzi
- Kusimamia upatikanaji wa majibu ya hoja za ukaguzi.
Majukumu ya Kitengo hiki ni kama ifuatavyo:
- Kutunza kaseti, magazeti, video, na filamu za Kiswahili
- Kuwasaidia watafiti na wanafunzi wa lugha ya Kiswahili
- Kuandaa na kusimamia taarifa, sera na taratibu za maktaba
- Kuanzisha na kusimamia utumiaji wa Mfumo wa Taarifa za Maktaba pamoja na huduma zake
Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
Majukumu ya Kitengo hiki ni kama ifuatavyo
- Kuandaa na kutekeleza mipango ya mwaka ya ununuzi na ugavi
- Kusimamia utekelezaji wa sheria na kanuni za ununuzi na ugavi Serikalini
- Kusimamia mchakato wa zabuni kwa kufuata taratibu zilizopo
- Kutoa taarifa za ununuzi za vipindi mbalimbali
- Kuandaa orodha ya vifaa vya ofisi