KAULIMBIU:  Kiswahili - Mhimili wa Umoja, Maendeleo ya Elimu na Uchumi.


Shughuli na Majukumu ya kila idara yameorodheshwa hapo Chini kama ifuatavyo:-


 1. Kuratibu, kusimamia na kuongoza shughuli za ukaguzi wa ndani.
 2. Kuongoza katika uchunguzi maalum wa fedha.
 3. Kushauri kuhusu mabadiliko ya miongozo ya Ukaguzi na kupendekeza mfumo mzuri wa udhibiti wa ndani.
 4. Kuandaa Sera kwa ajili ya shughuli za ukaguzi na kutoa maelekezo ya Sera hizo kiufundi na kiutawala.
 5. Kufanya tathmini juu ya ufanisi (effectiveness) katika ngazi zote za utawala kwenye Wizara/Idara/Mkoa unaohusika kuona ni jinsi gani wanasimamia mali (resources) na kuona kama taratibu zinafuatwa.
 6. Kufanya tathmini juu ya ufanisi (effectiveness) katika ngazi zote za utawala kwenye Wizara/Idara/Mkoa unaohusika kuona ni jinsi gani wanasimamia mali (resources) na kuona kama taratibu zinafuatwa.
 7. Kuidhinisha taarifa zilizochapwa kama matokeo ya shughuli za ukaguzi zilizofanyika.
 8. Kushirikiana kikamilifu na wa kaguzi wa Nje (CAG)
 1. Kumshauri Katibu Mtendaji kuhusu masuala ya ununuzi na ugavi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
 2. KKusimamia utekelezaji wa mpango wa ununuzi wa taasisi.
 3. Kusimamia utekelezaji wa mpango kazi wa taasisi.
 4. Kutengeneza kanuni na taratibu za stoo.
 5. Kuendesha mafunzo kazini ya usimamizi wa stoo.
 6. Kusimamia uhakiki Kmali ikiwemo mzunguko wa mali kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
 7. Kusimamia na kuratibu kazi za maafisa ugavi walio chini yake.
 8. Kufanya utafiti na kutoa ushauri ni jinsi gani gharama za ununuzi au utunzaji wa vifaa zinaweza kupunguzwa.
 9. Kushauri juu ya sera ya ugavi na ununuzi.
 1. Kuthibitisha vyanzo vya data.
 2. Kutunza vitabu vya mwongozo wa kuendesha kompyuta.
 3. Kusimamia mafunzo kazini.
 4. Kuhuisha tovuti ya Baraza
 5. Kufuatilia malipo ya mtandao
 6. Kuandaa mafunzo ya mifumo mipya ya kompyuta.
 1. Kusimamia uandaaji nyaraka kama vile mikataba na makubaliano mbalimbali yaliyoridhiwa na mwajiri.
 2. Kusimamia uandaaji mikakati ya ulinzi wa kisheria na uendeshaji wa kesi ambazo BAKITA litakuwa na manufaa nazo.
 3. Kutoa ushauri wa kisheria kuhusiana na majukumu ya BAKITA.
 4. Kuliwakilisha BAKITA katika masuala yote ya kisheria kama litakavyohitajika.
 5. Kusimamia uhifadhi wa umakini mkubwa nyaraka zote za kisheria za Baraza.
 6. Kusimamia utafiti wa kisheria unaohitajika na kuishauri menejimenti ya Baraza ipasavyo.
 1. Kutafsiri sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya kiutumishi na kutoa ushauri juu ya utekelezaji wake.
 2. Kusimamia mwongozo wa utayarishaji wa mpango wa muda wa kati na mfumo wa bajeti.
 3. Kusimamia sera za jumla na kuziratibu.
 4. Kuanzisha au kufanya utafiti wa masuala ya utekelezaji wa mipango.
 5. Kubainisha maeneo muhimu ya uwekezaji mali kwa kushirikiana na sekta mbalimbali.
 6. Kuratibu na kutoa ushauri juu ya masuala muhimu na matumizi bora ya undelezaji wa Sayansi na Teknolojia na matumizi yake.
 7. Kusimamia ufuatiliaji utekelezaji wa miradi/ programu za Baraza.
 8. Kusimamia ufuatiliaji utekelezaji wa sera mbalimbali za kisekta na kutoa ushauri.
 9. Kusimamia utekelezaji wa mikakati ya uwekezaji.
 10. Kusimamia uandaaji wa mapendekezo ya utafiti wa masuala yanayojitokeza katika Baraza.
 11. Kusimamia uandaaji wa mikakati ya mipango ya maendeleo ya muda wa kati na mrefu.
 12. Kusimamia utekelezaji wa dira ya Taifa kwa mwaka 2025.
 13. Kusimamia uratibu wa mwenendo wa misaada ya nje.
 14. Kusimamia uratibu wa mwenendo wa biashara yetu na nchi mbalimbali
 15. Anaweza kuteuliwa kuwa mkuu wa kitengo.