KAULIMBIU:  Kiswahili - Mhimili wa Umoja, Maendeleo ya Elimu na Uchumi.MAFUNZO YA KUTAMBUA VIPAJI VYA UKALIMANI


Imechapishwa Jumanne, 08 Oktoba 2019Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na wakalimani wabobezi litatoa mafunzo ya siku tatu ya kutambua vipaji vya ukalimani. Mafunzo yatatolewa katika mazingira yenye vifaa vyote muhimu vya ukalimani. Kila mshiriki atafanya ukalimani kwa vitendo na kufanyiwa tathminiya uwezo wake wa kukalimani.

Wakalimani watakaobainika kuwa na uwezo mzuri watatambuliwa rasmi na BAKITA na kuandaliwa mipango kabambe ya kuimarisha uwezo wao, ikiwa ni pamoja na kuanza kutumika katika kutoa huduma hiyo ya ukalimani.

Sifa za Mshiriki:

Kijana wa Kitanzania mwenye uwezo wa kuwa mkalimani katika lugha zifuatazo:
  1. Kiswahili –Kiingereza – Kiswahili
  2. Kiswahili –Kifaransa – Kiswahili
  3. Kiswahili – Kireno –Kiswahili
  4. Kiswahili – Kiarabu –Kiswahili

Gharama ya Kushiriki

Kila mshiriki atalipa shilingi laki moja na elfu thelethini tu (130,000/=) kwa ajili ya kuchangia gharama za kukodisha vifaa vya ukalimani, ukumbi na chakula kwa siku tatu za mafunzo.Malipo yatafanyika kupitia Benki ya NMB au kwa SIMU baada ya mlipaji kupewa namba ya kumbukumbu ya malipo.

Mahali, Tarehe na Muda wa mafunzo

Mafunzo yatatolewa katika Ofisi za BAKITA Kijitonyama, Tarehe 21– 23/10/2019 kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi 10.00 jioni.

Idadi ya washiriki:

Kutokana na vifaa tulivyonavyo, tutaanza na washiriki 25 tu. Kwa wale walio tayari kushiriki katika awamu hii ya kwanza tafadhali wasiliana na Mratibu wa Mafunzo, Bw. Arnold Msofe (0762 020227).