Tanzania emblem

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)

Tanzania emblem
Dondoo

Kuhusu BAKITA

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Shirika la Umma ambalo kwa kawaida huwa chini ya Wizara yenye dhamana ya Utamaduni. Baraza liliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 1983 na 2016. Sheria hii inalipa Baraza mamlaka ya kusimamia na kuratibu shughuli za wadau wote wanaokuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baraza liliundwa kutokana na mapendekezo makuu ya Kamati iliyoundwa kwenye kikao cha wataalamu wa lugha kilichoitishwa na Waziri wa Elimu Disemba 1961. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuinua Kiswahili kama lugha ya Taifa. Baraza lilianza kazi na watumishi wanne katika ofisi za Wizara ya Elimu. Miongoni mwa kazi ya kwanza ya Baraza ilipendekezwa iwe kufasiri msamiati na misemo ya Sheria. Baadaye mwaka 1972, Baraza lilipata ofisi zake katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa, mtaa wa Samora na Azikiwe jijini Dar es Salaam, na mwaka 2012 Baraza lilihamia Kitalu Na.45 B, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Huduma Zitolewazo na BAKITA

Huduma ya Ushauri kwa wanafunzi na watafiti

Soma Zaidi>>

Huduma ya Kutoa ithibati ya lugha

Soma Zaidi>>

Huduma za Tafsiri na Ukalimani

Soma Zaidi>>

Usambazaji wa Istilahi za Kiswahili

Soma Zaidi>>

Habari Mpya

  • 16th Oct 2023

“NIMERIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA BAKITA"- DKT. NDUMBARO

Soma zaidi
  • 13th Oct 2023

BAKITA LATAKIWA KUIBUA VYANZO VIPYA VYA MAPATO NA KUSIMAMIA MATUMIZI YA KISWAHILI FASAHA.

Soma zaidi
  • 10th Oct 2023

BAKITA LATEMBELEWA NA MABALOZI

Soma zaidi

Matangazo

Machapisho

Vitabu vya BAKITA

Maneno ya Mtandaoni

Neno: Damisi

Maana: Mtu Mchangamfu, mfurahishaji au mchekeshaji

Mfano:Mfano: Damisi alipewa zawadi

Neno: Afiriti

Maana: Mtu anayechochea wenzake kufanya uovu

Mfano:Afiriti amewasababishia wenzake kifungo

Neno: Belenga

Maana: Tembea kwa maringo na kujidai kwingi

Mfano:Mfano: Warembo wanabelenga jukwaani.